Spy Phone App ya:

Android

iOS

Watumiaji wote wa Simu pelelezi wanatakiwa kukubali masharti yote kwa ukurasa huu pamoja Mkataba wa Kisheria ya Mtumiaji wakati unapounda akaunti yako.

Masharti ya Huduma

Istilahi "tu-" au "sisi" or "-etu" inamaanisha wamiliki na wasimamizi wa tovuti hii na programu ya simu ya mkononi. Istilahi "u-" inamaanisha mtazamaji wa tovuti au mtu anayesajili na kutumia programu ya simu ya mkononi.


Kwa kufikia tovuti ya Simu pelelezi au kwa kusakinisha,kukimbiza au kutumia programu (Programu ya Android), unaonyesha shukrani na ukubaliaji wako wa masharti ya matumizi. Masharti haya yanaweza kubadilika. Ikiwa utaendelea kutumia tovuti au programu hii (Programu ya Android) baada ya mabadiliko,unakiri na kukubali mabadiliko hayo. Tafadhali soma masharti haya ya matumizi kwa mabadiliko yoyote.


Katika baadhi ya nchi ni kinyume cha sheria ya kusakinisha programu ya ufuatiliaji kwa simu ya mkononi ambayo wewe si mmiliki au huna idhini sahihi ya kusakinisha programu ya ufuatiliaji. Ni jukumu la mtumiaji kuheshimu sheria zote katika nchi yao. Kwa kupakua na kutumia programu ya Spy phone, unakubali kwa njia ya kupakua na kutumia programu hii na masharti yetu ya huduma:

-> Tafadhali angalia kwa makini sheria zote husika (jimbo, nchi, mkoa) kabla ya kusanikisha programu hii.
-> Simu pelelezi haijaundwa ili isiweze kugunduliwa.Ni lazima umjulishe mtu ambaye unamfuatilia. Programu ya Simu pelelezi imeundwa kwa ajili ya ufuatiliaji wa kimaadili ya watoto katika mchakato wa wazazi kudhibiti watoto wao au kwa waajiri ambao wanataka kufuatilia shughuli ya mfanyakazi wao.
-> Unaweza kusanikisha na kutumia programu hii kwa chombo ambacho ni mali yako, au ambacho una ruhusa ya kuandikwa ya kusanikisha programu,kutoka kwa mmiliki. Unapaswa kumjulisha yeyote anayetumia chombo ambacho programu hii imesanikishwa, afahamu ya kuwa shughuli yao kwa mtandao na simu inafuatiliwa na kuhifadhiwa kwenye nyaraka.


Tuna haki ya kufuta akaunti ya watu wanaokiuka kanuni ya Matumizi, na pia kutoa taarifa zao kwa wahusika wote (kisheria) kama njia ya kufuata sheria zilizopo.


Taarifa zote zinazokusanywa na programu hii haiwezi kutumiwa katika mahakama ya sheria.


Tunaidhinisha sera ya jumla ya usiri na faragha ya databesi ya mteja. Hatujawahi na hatutawahi kuuza maelezo kuhusu wateja wetu kwa "spammers" au wahusika wengine ambao wangependa kutangaza au kushawishi watu wanunue bidhaa zao au huduma. Programu yetu haikusanyi maelezo yoyote ya ziada kutoka kwa chombo chako kuliko yale yanayotakiwa kwa utendaji wake kwa ufanisi. Data yako ipo katika mikono salama.


Tunaweza kutuma maelezo muhimu kwa barua pepe uliyotumia kusajili (hii haitafanyika mara kwa mara). Kama utajitoa, hutaweza kupokea barua pepe zozote. Kwa kusakinisha programu kwenye simu, unakubali ya kwamba programu hii itakusanya data kutoka kwa simu hiyo na kuituma kwa seva yetu, ambapo utakuwa na uwezo wa kuutazama tu kama utaingia kwa kutumia la mtumiaji na nenosiri. Hatukusanyi nenosiri au namba za kadi ya mkopo. Tafadhali kuwa na ufahamu ya kwamba hatutakurudishia pesa kwa ajili ya kubadilisha nia yako. Kama unakabiliwa na matatizo ya kiufundi na programu yetu, tafadhali tutumie barua pepe na tutafanya kazi pamoja katika kukabiliana na / kurekebisha masuala haya. Kama hatutakuwa na uwezo wa kupata ufumbuzi wa kuridhisha na programu imethibitika kuwa mbovu, tutakurudishia pesa zako. Hatutakurudishia pesa kutokana na hali ambayo ulinunua programu hii na huna ufikivu kamili na yenye bila vikwazo kwa chombo ambacho kimepangiwa kufuatiliwa.


Hatutoi aina yoyote ya hati au dhamana kuhusu utendaji wa programu, uaminifu au uwepo kwa majukumu yoyote. Simu pelelezi haidhamini ya kwamba bidhaa, tovuti na maudhui yake na sifa zitafanya kazi bila kusumbuliwa au makosa, au kwamba utendaji wa bidhaa utakuwa bora zaidi kwa mifano yote ya simu. Matokeo yanaweza kutofautiana kulingana na sifa za kiufundi ya chombo. Kwa Android, unaweza kujaribu bidhaa hii kwa siku 3, bila malipoilikuitahini na kuamua kama inatimiza kazi iliyonuiwa.Kwa hali yoyote ile hatuwajibika kwa hasara yoyote ya upotevu wa data au uharibifu (kifedha, kimwili, kihisia au nyingine) ambayo inaweza kusababishwa kutokana na matumizi ya programu yetu.


Programu ya Simu Pelelezi na haki miliki zote (hataza na haki miliki) zinamilikiwa tu na Cad-Design. Kwa kununua programu tunakupa leseni ya matumizi isiyo ya kipekee na isiyoweza kubatilishwa, ya kuitumia, katika muundo wa mashine-someka. Leseni hii haikuhamishii haki zozote za umiliki au ushirika mwingine wa kisheria katika programu hii. Hutaweza kunakili,kurekebisha,kutafsiri ,kutosanya-zalisha, kukarabati,kufungua wazi msimbo na kujaribu kupata chanzo msimbo, kubadilisha, au kuunda programu yoyote kutokana na programu hii.


Alama za biashara ya Google, Android, Samsung, Whatsapp, Facebook, Skype, Viber, Line, si zetu. Alama yetu ya biashara Spy Phone App.